Billnas Afungukia Tuhuma Za Kuwa Mariooo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Billnas amefunguka na kukataa kata kata tuhuma alizorushiwa na Steve Nyerere kuwa ni mariooo.

Hivi karibuni Billnas na Steve Nyerere walijikuta katika vita kali ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Steve kumtuhumu Billnas baadhi ya mambo ikiwemo kuwa Marioo.

download latest music    

Billnas ameibuka na kukana taarifa hizo sio tu kwamba sio Marioo bali pia amemnyooshea kidole Steve na kudai inawezekana yeye ndio marioo maana anaonekana tu.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemwagia povu hili Steve Nyerere:

Mimi siwezi kuwa marioo halafu ukishawahi kusikia msemo “Anayesifia mvua ujue imemnyeshea” basi ndiyo yule ukiona mtu amezidiwa anakimbilia umarioo basi ujue yeye ana fanya huo umarioo.

Kwanza sina hiyo lifestyle ya kimarioo na siwezi kuwa Marioo ndio maana nina vitu kama Tagi Ubavu kwaiyo asiongee kitu ambacho hakijui”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.