Billnas: Sijashuka Kwenye Muziki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Billnas ambaye ametamba sana na kibao chake cha ‘Sina jambo’ amefunguka na kusema taarifa zinazodai kuwa yeye amefulia sio za kweli kabisa kwani hajatoa nyimbo yeyote tangu alipotoa ‘Sina jambo’.

Baada ya kukaaa kimya kwa muda mrefu  fununu zimeanzq kuzagaa kuwa mziki wa Billnas umeanza kushuka huku wengine wakidai Petit Man Wakuache kuondoka LFMG ndio kumesababisha hayo yote.

download latest music    

Billnas yupo chini ya uongozi unaoitwa LIve Fast LIve good (LGLF) na kwa muda mrefu Petit alikuwa manager wake lakini baada ya mikwaruzano na manager mwingine mwishoni mwa mwaka jana Petit aliondoka kwenye label hiyo na kusababisha Billnas kuwa chini ya uongozi mwingine kitu kilichowaaminisha wengi kuwa ndio Chanzo cha Billnas kushuka kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Billnas amekana tuhuma hizo na kufunguka yafauatayo:

Huwezi kusema nimepanda au nimeshuka kimuziki kwa sababu so far kwa sababu sijatoa ngoma yoyote at least wangesema hayo kama ningekuwa natoa nyimbo zinakataa bado naaamini niko juu na material ambayo niko nayo ni nyingi lakini anayeitwa hayo ni mawazo ya watu wengine siwezi kuwakataza kusema “.

Lakini pia Billnas amesema ukimya aliokuwa nao kwenye kutoa nyimbo ni kawaida yake sio kwa sababu hayuko na Petit Man lakini pia amesema ukimya huo kwenye game unatokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo ambapo anajishighulisha na biashara zake nyingine sio muziki tu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.