Billnass na Nandy Wabanwa Pabaya

Wasanii wa Bongo fleva Nandy na Billnass wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kubanwa na maswali kutokana na uhusiano wao.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi nying sana zilizotapakaa zinazodai ya kuwa mrembo Nandy au mwenyewe anavyopenda kujiita African Princess kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye gemu na wimbo wake wa sina jambo. Tangu tetesi hizo zimeanza kutapakaa wawili hao kila mmoja kwa wakati wake wamejitahidi kuficha au kakataa kabisa kuhusiana kimapenzi na kudai kuwa wana urafiki tu wa kawaida ambao unaweza ukauita wa kikazi.

download latest music    

Jana kupitia stesheni ya Clouds Fm katika kipindi cha XXL kwenye segment ya U heard, Soudy Brown aliwavutia waya Nandy na Billnass kwa kutaka kuwahoji kwa kile kilichodaiwa kuna kiwanja walionekana pamoja ingawa kila mmoja aliweka picha kwenye mtandao wa kijamii akiwa peke yake (yaani hawakupiga wote picha) lakini picha hizo ziliwaonesha wakiwa katika eneo moja wakila bata. Soudy alivyomuuliza Billnass alijibu hivi;

Mimi sina ukaribu na Nandy wala sijawahi kutembea naye yaani kwa ufupi hayupo hata listi ya watu niliowahi kutoka nao. Sijawahi hata kumfikiria kutembea naye yaani sijui kitu chochote kuhusu Nandy yaani ukiniuliza kuhusu huyo mtu unakuwa unapotea’.

Baada ya kumuuliza Billnass na yeye kukana na kumruka futi 100 Nandy ikabidi tu ampigie na Nandy ili apate ukwdeli wake;

Unajua watu wanasema hivyo kwa sababu tulipiga picha kiwanja kimoja lakini sio ukweli mi nilienda na dada yangu na rafiki angu anaitwa Vai sina sababu ya kuficha kama ningekutana naye siningesema sina haja ya kuficha”.

Kila mmoja amesisitiza hatoki na mwenziye na kila mmja ni bachela lakini kama wanaendana fulani enhee??

Lakini anyway wazungu wanasema time will tell yaani muda ndo utasema alafu isitoshe mapenzi hayafichiki.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.