Billnas -“Nandy Ana Sifa Zaidi Ya 60% Za Mwanamke Wa Kuoa”

Ikiwa ni  muda sasa tangu kuwepo kwa  tetesi za wasanii wa Bongo Fleva Nandy na Billnass kusemekana kuwa wapo katika mahusiano ya kimapenzi, Billnass nae ameamua kusema yaliyopo moyoni kuhusu mrembo huyo ambae amekuwa akifanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii huyo wa kiume alipokuwa katika mahojiano na BongoSwaggz alisema kuwa katika mipango yake ya kimaisha kwa sasa bado hana mpango wa kuoa ingawa atategemea kuoa hapo baadae, lakini bado alisema kuwa hata muda wa yeye kuoa ukifika bado kuna vigezo ambavyo anavizingatia hivyo muda ukifika laziamataangalia vile vigezo vya kumfanya aoe.

download latest music    

Billnass ambae amekuwa akifanya vizuri katika game la muziki kwa muda mrefu sasa huku nyimbo zake nyimbo zake karibia zote zikipokelewa vizuri na mashabiki,kwa sasa Billnass anatamba na vibao vyake vya  ‘mazoea’ na ‘sina jambo’ ambayo imetolewa hivi karibuni.”sijakaa nikafikiria  kwa sababu na mimi nina vigezo vyangu  ambavyo nataka , najua namtaka  .Najua namtaka mwanamke wa aina gani .Kwanza swala la kuoa kwangu linapita mbali,sio kwamba ninafikiria sana” ameongea Bilinass

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu msanii  mwenzie wa kike wa Bongo Fleva  ambae kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa wapo katika mahusiano naye na wamekuwa wakionekana baadhi ya sehemu pamoja msanii Billnass anasema kuwa Nandy ni mmoja wa wanawake anaowapa zaidi ya 60% kwamba anasifa na vigezo ambae yeye anavihitaji  kwa mwanamke wa kuoa.

Nandy ni mwanadada ambae anafanya vizuri sana kwa sasa katika game akiwa ni msanii chipukizi aliechukua nafasi kubwa sana hasa mwaka 2016, lakini bado anaendelea kufanya vizuri kutokana na nyimbo zake kupendwa na mashabiki pia,Nandy kwa muda sasa amekuwa  akifanya vizuri na nyimbo zake kama ‘nagusagusa’ , ‘one day ‘na huo mpya wa ‘wasikudanganye’,pia amepata bahati ya kuwepo katika tamasha la Cokestudio kwa mwaka 2017.Lakini pia Nandy ni mjasiriamali ambae ana Lebel yake ya ushonaji wa nguo inayojulikana kama Nandy African Print. Kwa sifa za kujituma na kufanya kazi inawezekani ndipo aslimia 60 ya billnass inapokuja kwa nandy.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.