Bob Junior Anasakwa na Polisi Baada ya Kumtembezea Kipigo Cha Mwizi Mpenzi Wake Sabrina

Mwanmuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Bob Junior amekumbwa na skendo mpya ya kumpa kipigo cha haja aliyekuwa mpenzi wake Muigizaji wa Bongo movie Sabrina au maarufu kama Sabby angel.

Sabrina na Bob Junior wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka zaidi ya nane ambapo inadaiwa Bob Junior amekuwa naye Kwenye Mahusiano hata kabla ya kuoa na inadaiwa hata baada ya Kumuoa aliyekuwa mke wake Halima aliendelea kuchepuka na Sabby.

download latest music    

Kwenye Interview aliyofanya na Shilawadu ya Clouds Tv, Sabby amefunguka na kudai Bob junior amempiga kipigo cha mwizi baada ya kumwambia anataka kuvunja Mahusiano yao kwani alikuwa haoni kama wana future pamoja.

Baada ya habari hizi kuenea Shilawadu walimtafuta na kumuuliza kama ni kweli alipoweka na Bob Junior Sabrina alifunguka:

Kweli kuna matatizo yametokea, unajua mtu huwezi kulazimisha mapenzi nikikwambia it’s over its over lakini yeye anaforce mapenzi ananipiga mambo ya zamani kwanza siku hizi mwanamke hapigwi unanipiga umenitolea mahari? Nimeona hana future nikaamua kumuacha lakini mtu hataki kuelewa anakuja ananipiga mi naona kama naonewa”.

Sabrina ameelezea kuwa Bob Junior Alifika nyumbani kwa ndugu yake na kuanza kumlazimisha kuondoka naye baada ya yeye kukataa Akaanza kumpiga Ngumi, Mateke akamkalia na kumuumiza vibaya mno.

Sabrina aliweka wazi kuwa aliamua kumuacha Bob Junior kwani ni mtu ambaye hafikirii maendeleo yeye anapenda kufanya starehe na kunywa pombe wakati yeye anataka maendeleo.

Sabrina ameweka wazi kuwa Bob Junior anasakwa na polisi kwa hivi sasahivi maana ana RB yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.