Bob Wine Arejea Kutoka Marekani Kaka Yake Atiwa Mbaroni

Msanii wa muziki kutoka Uganda na Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amerejea kutoka kwenye matibabu nchini Marekani lakini kaka yake ametiwa mbaroni.

Kaka wa Bobi Wine, Eddy Yawe amekamatwa asubuhi ya leo na maofisa wa uwanja wa ndege wa Entebbe alipokuwa anaelekea kumpokea mdogo wake.

download latest music    

Vyombo vya habari nchini vinaripoti kuwa Mashuhuda wamesema Yawe alikataa kuandika taarifa ya polisi akisema alikuwa anamsubiri mwanasheria wake.  Haikufahamika ni kwa nini alitakiwa kuandika taarifa hiyo.

Bobi Wine alitegemewa kuwasili uwanja  wa kimataifa wa Entebbe saa nne asubuhi hii.

Wakati huohuo, polisi wameizingira nyumba ya mwanasiasa wa upinzani, Meya Erias Lukwago.

Pia,  nyumba ya mbunge wa Makindye Magharibi,  Allan Sewanyana, imezungukwa na polisi ambao hawajasema ni kwa nini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.