Bright Awaumbua Alikiba na Diamond,Asema Hawajulikani S.A

Msanii wa kizazi kipya ambae alikuwa akitamba sana tangu ametoa nyimbo zake zaidi ya tatu mfululizo na kupokelewa vizuri na mashabiki bright ameamua kuwaumbua na kuwalipua wasanii wakubwa bongo diamond na alikiba kwa kusema kuwa hata wao ni wasanii wa kawaid a sana wanapofika Afrika ya Kusini na wakati hata hawajulikani sana kama vile watu wanavyofikiria.

Bright ambae alikuwa South Afrika siku za hivi karibuni alisema kuwa hata alipokuwa akitembea baadhi ya sehemu na kwa anawauliza watu kama wanawafahamu wasanii kutoka Tanzania kwa kuwatajia jina la Alikiba na Diamond, watu wa kule walikuwa wakikataa na kusema kuwa hawawajui watu hao.

download latest music    

Wakati nipo kule South africa,nilikuwa nikiwauliza baadhi ya mashabiki kaama wanawafahamu wasanii wa hku kwetu,niliwauliza kama Diamond wanamjua wakasema hawamju na Alikiba pia.

Hata hivyo Bright alisema kuwa kwa upande wa wabongo wamekuwa wakiwajua wasanii watanzania sana lakini ukizungumzia wazawa wanaowajua diamond na alikiba sio wengi kama ambavyo watu wanavyofikiria kujulikana kwa wasanii hao nje ya nchi.

Hata hivyo Diamond na Alikiba wamekuwa wasanii wkaubwa na wamejitahidi kutengeneza fan-base kubwa afrika na duniani kwa ujumla, inaezekana kuna baadhi ya maeneo wasanii hao wasijulikane sana kama sehemu nyingine .

Ingawa bado haijulikanai kwanini Bright alikuwa akitaka kujua kujulikanakwa wasanii hao nje ya nchi kungemsaidia nini lakin pia hii inaweza kuwa changamoto kwa wasanii wenyewe kuwa bado wanakazi kubwa ya kuwafanya mashabiki wawajue na kupenda muziki wao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.