Bright:Sijawahi Kujiingiza Katika Mapenzi,Sijui Kuumizwa

Msanii wa  muziki anaefanya vizuri kwa sasa katika anga hizo Bright ambae sasa hivi ana kibao chake kipya cha Sina, ameiambia Clouds 360 kuwa hajawahi kujiingiza katika mapenzi wala hajui chochote kuhusu mapenzi kwaio hana chochote anachojua kuhusu kuumizwa na mapenzi.

Bright alipoulizwa kwanini muda mwingi amekuwa akiimba nyimbo zinazouhsu mapenzi , amesema kuwa kwa upande wake nyimbo anazokuwa anaimba ni kazi ya sanaa lakini haihusiani kabisa na maisha yake halisi ya muziki.

download latest music    

sijawahi kabisa kujiingiza na maswala ya mapenzi,kwaio sijui chochote kuhusu kuumizwa na mapenzi mimi ninafanya tu kazi ya sanaa kuimba nyimbo za mapenzi.kupenda hiyo ipo kama binadamu ni kawaida mtu anapedna lakini bado sijajiingiza katika mapenzi na siku nikiwa katika mahusiano kabisa mtajua tu kuwa nina mahusiano.

kuhusu zile picha za beach nikiwa na mdada zilikuwa ni picha za video, tulikuwa location

Mwanamuziki huyo akiendelea na mahojiano hayo alisema kuwa kufanukiwa kwake kimuziki kunatokana na ndhamu yake ambayo inatokana namalezi aliyoyapata kutoka kwao.pia bright anasema kuwa katika kazi zake zote hakuna hata nyimbo moja ambayo amewahi kuandikiwa ingawa hakitokea mtu akamwandikia hawezi kuacha kuimba.

tangu nmeanza muziki sijawahi kuandikiwa mashairi,nyimbo zangu zote nimekuwa ninaziandika mwenyewe ila ikitokea mtu ananiandikia na nikaupenda wimbo nitafanya kazi.

Kwa kuongezea pia bright ansema kuwa kwa sasa anjiusisha na kilimo cha mpunga na mahindi huko mkoani Morogoro ambako ndipo alipokulia na kusoma huko huko.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.