Chambuso Aongea, Msanii Wake Hapendi Kushindanishwa.

Meneja wa msanii mkubwa wa bongo fleva Chambuso amefunguka na kusema kuwa msanii wake ( Aslay) hapendi kushindanishwa na msanii yoyote kwa sababu watu wanatofautiana katika ufanyaji kazi na kuwashindanisha kunaleta tension kubwa kwa mashabiki.

Chambuso anasema kuwa Aslay haimbi ilikupata sifa kutoka kwa mtu yoyote ila anafanya kazi kwa sababu ni kazi yake hivyo hapendi anapoona watu wanakuwa wanamlinganisha na wasanii mwingine.

download latest music    

Maneno ya meneja huyo yanakuja baada ya kusambaa kwa maneno katika mitandao ya kijamii kwamba msanii huyo kwa sasa ameanza kushuka kwa sababu hatoi nyimbo nzuri kama zamani, huko wakijitahidi kumlinganisha na wasanii wengine na kumwambia kuwa kuna wasanii wenye vipaji vidogo lakini sasa hivi wameanza kumpita katika kazi za muziki.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.