Chemical Akanusha Taarifa za Kufulia Kimuziki

Msanii wa kike wa hip-hop nchi chemical amekanusha tetesi zinazosambaa zidi yake kuwa kwa sasa amefulia kumizki na ndio maana amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo wowote.tetesi za kufulia kwa Chemical zinakuja baada ya kuwa kwa kpindi hiki kifupi kuna wasani wengi wa kike wanaofanya muziki kama wake wameibuka na wamekuwa wakifanya vizuri hivyo Chemical amewekwa chini na wanadada wenzake.

Lakini hata hivo akijibu tetesi hizo , Chemical anasema kuwa mashabiki wake wengi wamekuwa wakihisi kama amefulia kwa sababu ya kuwa amejikita sana katika kufanya muziki wa singeli  na kuacha muziki uliomfanya ajulikane sana kwa mashabiki wake.Hata hivyo akiongea kwa kujitetea Chemical amesema kuwa kufanya singeli kwake sio kufulia bali alifanya ili kuwaonyesha mashabiki kuwa anauweoz wa kufanya muziki tofauti tofauti.

download latest music    

Siwezi kufulia hata siku moja kwa sababu mimi chemical ni kiwanda kwa sababu kinajitosheleza kwa uzalishaji wa muziki wa muziki, kwaio watu wanaodhani kuwa nimefulia  wanakosea sana  na kiukweli wategemee kuona mambo makubwa na mazuri kutoka kwangu.-Alisema Chemical huku akiwaahidi mashabiki kuwa anakuja vizuri kimuziki.

Chemical ambae kwa hivi karibuni amekuwa akifanya vizuri na wimbo wao mpya alioshirikishwa na mwana hip-hop mwenzie Pink ambao umekuwa ukifanya vizuri sana katika vyombo mbalimbali.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.