Chid Benz akamatwa na watu sita wengine kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amedhibitisha kuwa watu saba walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Hamduni alisema kuwa msanii Chid Benz alikuwa miongoni mwa watu hao saba ambao walikamatwa wakiuza dawa za kulevya aina ya Heroine.

download latest music    

“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema kamanda Hamduni.

Chid Benz

Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Chid Benz amekamatwa mara kadhaa kwa tuhuma za kujihusisha na utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. Staa huyo alishikwa Oktoba 24, 2014 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere