Chid Benz Aomba Asivunjwe Moyo, Asipuuzwe.

Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amewataka watu kumsikiliza anayosema bila kumuhukumu kwa udhaifu wake.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Chid Benz amesema kwamba mara nyingi amekuwa akiongea mambo ya msingi, lakini watu wamekuwa wakimpuuza na kumchukulia kama mtu aliyedata, huku vijana wengine wakiendelea kupotea.

Chid Benz ameendelea kusema kwamba hata kama wanamuhukumu kutumia madawa ya kulevya, lakini wasiangalie madawa anayotumia wala udhaifu mwingine, bali wachukue maneno anayoyazungumza ili kuokoa wengine.

download latest music    

Ukiskiliza interview zangu jinsi ninavyozifanya na mood zinavyonikuta, zimegeuzwa kama masihara ila kitu kama mtu anasikia na anasema huyu jamaa anaongea nini!?. Tuchukulie kavuta bangi, toa bangi zake, tuchukulie anakula unga, toa unga wake, ila fikiria anaongea nini!?”,  “Chid alikuwepo kama miaka 15 kwenye hii ‘industry’ nazunguka zunguka, wakati mwingine naona bora ninyamaze kwa sababu mimi nikiongea watu wanachukulia kama nimedata, lakini watu wengine wanazidi kupotea, wanazidi kufa wanazidi kukosa hela, wanazidi kuwa wajinga, wanazidi kuwa wapumbavu, wanakaa magetoni mwao wanasema Chid Mjinga, bangi tu”, amesema Chid Benz.

Hivi karibuni Chid Benz amekuwa akisema mambo mbali mbali kuwasema wasanii wenzake, jambo ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakimdhihaki kutokana na uraibu ambao alikuwa nao miaka ya hivi karibuni.Pia aliwahi kusema tayari amefanya collaboration na 2pac

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.