Chidi Benz azungumza kuhusu ishu ya kukamatwa na dawa za kulevya

Mwanamziki Chidi Benz sasa hivi yuko huru baada ya kudaiwa kukamatwa na polisi baada ya kupatikana na madawa ya kulevya hivi karibuni.

Akizungumza na showbiz Etra ya bongo, Chidi Benz alidai kuwa kwa sasa hana ruhusa ya kuzungumzia ishu hiyo huku akisema kuwa vijana wanapaswa kuwacha kwani zikona madhara yake.

download latest music    

Tazama mahojiano yao hapa kwa hisani ya Showbiz.

Showbiz Extra: Sawa, na hili la wewe kukamatwa na dawa za kulevya liko vipi? Ni kiki ya kutoka na video ya wimbo au kuna ukweli upi ambao umejificha ikizingatiwa wewe umewahi kukiri mara kadhaa kuachana na dawa za kulevya?

Chid Benz: Kuhusu hilo nina ushauri kutoka kwa mama watoto wangu kwamba nisilizungumzie zaidi. Lakini kwa ufupi ni kwamba mtu kukamatwa na dawa za kulevya ni sawa na mtu aliyekamatwa na bangi, mirungi ama chochote kile ambacho kinaonekana kuvunja sheria za nchi! Kwa hiyo nisiingie huko sana lakini jambo la msingi ni kwamba vijana wa Kitanzania wasijaribu na wanaotumia dawa za kulevya waachane nazo, siyo nzuri zaidi wajenge taifa kwa manufaa ya kizazi chetu.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua