Christian Bella Awatolea Povu Zito Wasanii Wenzake

Mwanamuziki mahari wa mziki wa dansi nchini Christian Bella amewatolea povu zito wasanii wenzake wa muziki wa dansi ambao wamekazana kumsema na kudai hana uwezo mkubwa wa kuimba bali anabebwa sana na vyombo vya habari.

Kwenye kila mapambano huwezi ukakosa watu ambao wataenda tofauti na wewe kwenye mapambano ya Christian Bella kuna baadhi ya wasanii wenzake wa Muziki wa dansi ambao wanampiga mawe na kusema uwezo wa Bella ni mdogo lakini amekuwa akibebwa sana na media kwa nyimbo zake kupewa upendeleo na kuchezwa zaidi.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Bella ameshindwa kuwavumiloa watu hao na ameishia kuwatolea povu zito kuonyesha kuwa amechoshwa na majungu ya wasanii wenzake ambapo amezidi kufunguka yafuatayo:

Wadau wa muziki wa bendi wanasema labda anabebwa labda nyimbo mbaya au labda ya kawaida sasa unataka nyimbo itoke mbinguni? hakuna kitu special ambacho hakijawahi kifanyika kila kitu kilichafanyika mziki ulishafanyika wahenga walishaimba lakini melody ndio tofauti. Yaani akisema Christian Bella anabebwa ni muongo sana Tena ana wivu wake binafsi alafu mimi sina mzunguko kwenye media mimi nikitoa wimbo nazunguka kwenye vyombo vya habari hakuna kitu kama hicho”.

Christian Bella amesisitiza kuwa sababu pekee nyimbo zake zinapigwa ni kwa sababu ya mziki mzuri anaofanya lakini hatumii nguvu nyingi kama wasanii wengine na hivyo wasanii wa dansi wanaomsema anapendelewa ni wana wivu naye.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.