Loading...

Chuchu Hans Amkingia Kifua Wema Sepetu Kuhusu Mtoto

January 22, 2018 at 08:39
Chuchu Hans Amkingia Kifua Wema Sepetu Kuhusu Mtoto

Msanii wa bongo movies Chuchu Hans na msanii mwenzie Ray Kigosi waliamua kuonyesha sura ya mtoto wao wa kiume ambae jana alitimiza mwaka mmoja na  ndio ilikuwa ni kwa mara ya kwanza mtoto huyo kuonekana katika mitandao ya kijamii tangu azaliwe.

Hata hivyo baada ya kuonyesha sura ya mtoto huyo wasani wengine walivutiwa na muonekanao wa mtoto huyo hivyo wengi walimpost mtoto huyo katika page zao za instagram na ndicho alichokifanya Wema Sepetu lakini hali ilikuwa tofauti katika page hiyo ya mwanadada huyo kutokana na  mashabiki wengi kuanza kumshambulia mwanadada Wema Sepetu  kuhusu tatizo lake la kutopata mtoto huku wengi wakimtuhumu na kumtukana kuwa chanzo cha  kukosa mtoto  ni yeye mwenyewe.

Loading...

Chuchu Hans aliumiza na maneno yaliyokuwa yakimlenga Wema Sepetu hivyo alifunguka na kuwaomba mashabiki kumuacha Wema aishi kwa amani kwa sababu maumivu ya kutafuta mtoto na kukosa ni makubwa sana  hivyo wanavyokuwa wakiendelea kumtukana  na kumuandana wanakuwa wanamuumiza sana.

ninasikitika sana kuona watu wanaongea maneno kibao kwa wema tena inawezekana wengine hawajazaa bado na wengine wameshazaa,…naomba nitoe historia yangu kidogo.mimi jaden sio mtoto wangu wa kwanza lakini kabla sijampata jaden nilikuwa napata maumivu sana kwa sababu zilishaharibika mimba kama tatu na nilikuwa nasikia maumivu sana na ukumbuke kuwa hakuwa mtoto wangu wa kwanza….

Hata hivyo ChuchH hans amewataka watu wanaomshambulia Wema wakae na kufikia kama wao ndio wamngekuwa Wema ingekuwaje, anasema kuwa kabla hajazaa na Ray wengine walisema kuwa Ray hana kizazi na hawezi kuzalisha lakini leo wanamtoto tayari.

muwe mnavaa viatu vya mtu na wala mapungufu yake isiwe fimbo ya kumchapia.watu waliongea sana kuwa baba jaden hazai, na miungu watu waliongea sana lakini kwa Mungu kila kitu ni kidogo.

Kwa muda mrefu sana wema amekuwa akitafuta mtoto na hata kupata mimba  na zingine kutoka , lakini watu wamekuwa wakimsema vibaya  na kum-judge tofati bila kujua maumivu anayoyapata msanii huyo.

 

Share

Comments

  1. Bongo hii kuishi stress tupu

  2. Wamwache tu aishi maisha yake

  3. Inakera sana

  4. Kila issue imekua kero hata watoto?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…