Coyo Anaonyesha Hisia Zake Kwa Vannesa,Atamani Mkewe Awe Kama Yeye

Msanii wa muziki wa bongo fleva  Coyo ,ambae sasa hivi anatamba na kibao chake cha Nyakanyaka  amefunguka wazi na kuonyesha hisia zake kwa mwanamuziki wa kike vannesa mdee na kutamani kuwa mwanamke aliye nae awe kama Vannesa kutokana na sifa nzuri alizonazo msanii huyo hasa kujituma katika kazi na kutambua ni nini anafanya.

Coyo ameongea hayo alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha the playlist na kusema kuwa katika wasanii wa kike wanaofanya vizuri na kuijituma basi vannesa mdee ni namba moja na hawezi kufananishwa na msanii mwingine , lakini pia Coyo anasema kuwa Vannesa ni msanii anayefanya kazi kwa kujua ni nini anafanya na amekuwa mwanamke hasiye kuwa na skendo sio kama kina Gigy Money.

download latest music    

Vee anaonekana ni mtu mwenye future ambaye ana mipango , kiufupi ni mwanamke ambaye anajituma kuanzia kwenye  kazi zake na anajua ni kitu gani anafanya, kwaiyo huwa namkubali sana natamani hata wangu angekuwa  kama yeye lakini asiye na skendo kama za Gigy Money .

Hata hivyo Coyo alionekana kutokuwa na wasiwasi wa kumuongelea Gigy Money kwa kumchana na tabia hiyo ya kuwa na skendo na kuongezea kuwa

kitu kizuri kama kiki chenyewe siyo utafute kiki,kuna kitu kimekiki,kuna kitu kimetafuta kiki  na kuna kitu kinatafutiwa kiki , hivyo ni vitu vitatu tofauti.-Aliongezea Coyo akimaaanisha kuwa Gigy Money ni mwanamke anafanya skendo hili kutafuta kiki.

Vannesa Mdee ni moja ya wasanii wa kike kwa sasa ambao wamekuwa wakifanya vizuri na inawezekana akawa ndio msanii wa kike ambae anaongoza kwa kufanya nyimbo nyingi na wasanii wa nje kwa miaka hii miwili ya hivi karibuni, ukiachana na kufanya vizuri na kupendwa bongo lakini pia Vannesa amejitahidi hata kufungua soko lake la muziki hata kwa nchi za nje na amepokelewa vizuri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.