Cyrill Kamikaze Aweka Wazi Uhusiano Wake Wa Kimapenzi na Feza Kessy

Mwanamuziki wa Bongo fleva Cyrill Kamikaze amefunguka na kuanika uhusiano wake wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzie mwanadada Feza Kessy.

Uhusiano wa Feza na Cyrill ulishika vichwa vya habari na kutapakaa kwenye mitandao ya kijamii mapema wiki chache zilizopita mara baada ya Cyril kurusha picha mtandaoni ya Feza iliyomuonesha akiwa kifua wazi jambo lililowakera mashabiki wengi na hivyo kumjia juu.

download latest music    

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa, kupitia kipindi cha Friday Night Live Cyrill amefunguka yafuatayo kuhusu mapenzi yao yeye na Feza;

Mimi na Feza kwa mara ya kwanza tulikutana Arusha mwaka 2011 ambapo nilimuona nikavutiwa naye tukawa marafiki na mpaka sahivi tuko pamoja, ni wapenzi ingawa watu wengi wanamuona kama mgumu fulani kwa mavazi yake ya kiume lakini sio mda wote anavaa hivyo au anakuwa hivyo, lakini pia kilichonifanya nimpende Feza kwanza kabisa ni msichana mmoja mkarimu sijawahi ona pili ni mzuri sanaaa tatu ni msichana mmoja mchapa kazi yaani ni demu mtafutaji na ni mkweli”.

Feza alipata umaarufu baada ya kushiriki mashindano ya Big Brother Africa yaliyofanyika mwaka 2013 lakini pia kabla ya hapo aliwahi kushiriki mashindano ya urembo na pia hivi sasa ameingia kwenye mziki wa Bongo fleva ambapo ametoa nyimbo chache lakini pia ni mtangazaji wa kituo cha Choice FM.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.