Diamond Aandamwa Tena ,Tetesi Mpya Zaibuka.

Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu msanii  mkubwa wa Bongo Fleva nchini kuamua kufunguka katika vyombo vya habari na kusema na kukiri ukweli juu ya tuhuma nzito zilizokuwa zikimuandama juu yake kuhusu yeye kutelekeza mtoto aliyezaa na video queen maarufu nchini,Hamisa Mobeto .Msanii huyo alisema ukweli kuwa mtoto huyo ni kweli wa kwake na sio kweli alikuwa haihudumii ila tu aliamua kufanya siri kwa sabbu kuna vitu alitaka kuviweka sawa ilhali msanii huyo tayari anafamilia yenye  watoto wawili.

Jana Septemba 21, katika mitandao tena kumeibuka kwa tetesi nyingine mpya ambazo hazizathibitishwa na pande zote mbili kuwa Diamond alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Miss Burundi mwaka 2012, hata hivyi taarifa hizo zinadai kuwa mlimbwende huyo ana watato wawili mapacha  aliozaa na msanii huyo mkubwa nchini na aliamua kuitelekeza mimba ya watoto hao mara tu alipojua habari hizo.Hata hivyo katika ukurasa huohuo wa instagram   huyo anaelezea jinsi yeye na Diamond walivyokutana Burundi alipokuwa kwenye show, na kipindi icho Diamond alikuwa bado hajakutana na Zari ambae ndio mama wa watoto wake wawili.

download latest music    

Kwa mujibu wa mwandishi wa ukurasa huo wa Instagram , anaeleza kuwa hata mama wa watoto wa Diamond anamjua yeye na anajua kuwa ana watoto wawili mapacha ambao amezaa na msanii huyo, akionekana kuandika kwa shida lugha ya kiswahili aliandika kuwa watoto hao mapacha ni wa msanii Diamond na msanii huyo amewakataa.

Ingawa imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wasanii kukutwa na tetesi za kutelekezwa  watoto lakini inakuwa kama tofauti kwa  Diamond kwa sasa kutokana na swala la kifamilia ambalo limetokea hivi karibuni.Tangu tetesi hizo zitokee msanii huyo hajaamua kusema chochote ukizingatia ni taarifa zilizozuka tu katika mtandao wa Instagram.katika  interview yake Diamond alikaririwa  akisema kuwa mtu yeyote anaejiamini kuwa mtoto aliyenae amezaa na yeye basi amlete na yeye atakubali.

Hata hivyo kama kawaida ya watu wa  mitandao , maneno uwa hayakosekani, wameendelea kumtuhumu na kumtupia maneno msanii huyo bila kuwepo na uhakika wa taarifa hizo huku wakifananisha watoto hao na mtoto wa kike wa kwanza wa msanii huyo.Nadhani ni wakati wa kusubiri ili msanii huyo aweze kufunguka kuhusu taarifa hizo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.