Diamond Adaiwa Kuvunja Ndoa Ya Mtangazaji

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta Tena Kwenye headlines kwa mambo ya Mapenzi baada ya kukumbwa na skendo mpya ya Kuvunja ndoa ya Mrembo ambaye ni mtangazaji.

Global Publishers wanaripoti kuwa kwa muda sasa kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa Mahusiano ya kimapenzi kati ya Diamond na Mrembo ambaye ni mtangazaji wa Channel 10 aitwaye Zein Aklan amayetangaza kipindi cha Profile na Style

download latest music    

Taarifa za skendo hiyo ya Diamond na mke wa mtu imeenea Kwenye mitandao ya kijamii ambapo inadaiwa wawili hao walikutana Mrembo huyo alipoenda kufanya kazi ya kuwapamba WCB.

Baada ya Tetesi hizo GPL lilimsaka Mrembo huyo ambaye alikataa taarifa man kukiri kuwa ndoa yake ipo matatani kwani mume wake aitwaye Arif Aklan hataki kumuelewa kwanini awekwe Kwenye skendo hiyo:

Yaani hapa nilipo nipo kwenye tabu kubwa sana na mume wangu kwa sababu haelewi ni kitu gani hiki na isitoshe hajawahi kuona mambo kama haya kwenye mtandao tangu tumeishi hivyo habari hizo zimeleta mtafaruku mkubwa sana.

Ndugu wa mume wangu nao hawanielewi na mimi sijaachana na mume wangu kama watu wanavyosema mitandaoni, naumia jamani maana habari hizo hazina ukweli na zimeniweka kwenye wakati mgumu sana”.

Lakini pia mrembo huyo amewaomba watu wanaosambaza habari hizo ambazo hazina ukweli waache mara moja maana watavunja ndoa yake:

Nawaomba wanaosambaza skendo hiyo waache jamani maana ndoa yangu inaweza kuvunjika wakati wowote kwa sababu ya kitu ambacho hakina ukweli wowote, sina hata mazoea ya kivile na Diamond”.

Mrembo huyo amesisitiza kuwa hajawahi kufanya kazi na Diamond ingawa wanafahamiana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.