Loading...

Diamond akiri kuzaa na Hamisa Mobeto

September 19, 2017 at 12:18
Diamond akiri kuzaa na Hamisa Mobeto

Hatimaye  msanii mkubwa wa Bongo Fleva nchini Diamond Platinumz ameamua  kusema ukweli kuhusu tetesi zilikuwa kuwa zikisambaa mitandaoni  kuhusu ujauzito wa mwanadada video queen maarufu nchini Hamisa Mobeto.Diamond amesema ukweli baada ya kuenea kwa picha na video clips nyingi mitandaoni zikimuonyesha akiwa kitandani na mwanadada .

akiongea katika kipindi cha leo tena Cha clouds tv, Diamond amekiri kuwepo na mahusiano kati yake na Hamisa kipindi cha nyuma na hapo katikati walirudiana ilhali mrembo huyo akijua  kuwa Diamond ana familia .

Loading...

“Mimi na Hamisa tulikutana tangu mwaka 2010, tukawa na mahusiano lakini mahusiano yetu hayakudumu, kipindi icho nilikuwa sijakutana na Wema wala Zari.” akiri diamond “kipindi nipo na zari alianza kunirequest turudiane  lakini nilimwambia mimi nina familia tayari,tukaendelea..baada kama ya siku tatu habari zikaanza kusambaa mitandaoni Diamond anatembea na hamisa” amesimulia.

‘Baada kama ya miezi alinipigia simu kuwa  ana ujauzito wangu, basi nikamuuliza yeye ameamuaje, nikamwambia sawa ila mimi nina familia yangu , nilikubali na nikaanza kulea ujauzito wangu” amekiri diamond

“Mpaka mimba inakuwa , kila siku alikuwa anapokea si chini ya elfu sabini kwa siku,na hata mimba ilikuwa kubwa nilimnunulia Rav4, na tushakubaliana tukae kimya ,sikuwa tayari kuzungumzia swala ilo kwenye media”

Baada ya kuona maneno yanazidi katika mitandao Diamond aliamua kumwambia ukweli mzazi mwenzie zari na kukiri kosa lakini alimwambia hamisa hana haja aya kumtukana zari na watoto wake maana watoto watachukiana wakati wote ni wake.

Diamond anasema kuwa alikuwa akimuhudumia hamisa, na hata alipoenda kujifungua aliacha zaidi ya mil7 kwa ajili ya shopping ya mtoto na bado akampa ela kwa ajili ya kujifungua, anakiri kuwa ni ujinga wake ndo ulifanya yote yakatokea  “familia yangu imetukanwa kwa sababu ya ujinga wangu.. nilitoka uingereza usiku nikaenda kulala na mtoto wangu ”

Diamond anakiri kuwa alikuwa karibu na Hamisa kwa sababu alikuwa anaamini kuwa mtu anapokuwa na tumbo(ujauzito) hapaswi kujisikia vibaya.hata hivyo Diamond ameomba radhi kwa familia yake, watoto wake na mama mzazi wa watoto wake Zari.

 

 

Share

Comments

  1. Kaliiiiiii nyoooooo bure yake sasa ndo anampost maana siri iko waziii

  2. pambanaa na hali yako

  3. Naanza punguza ushabiki kwako mfyuu

  4. Simbaaa mtoto

  5. Hongera Sana Sana Nimefurah hadi chozi

  6. Safi sana kaka ukojuuuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…