Diamond Alikuwa Ananipa Gundu;-Hamisa

WANAMITINDO anayebamba Bongo, Hamisa Mobeto amekiri kuwa mzazi mwenzake ambaye ni mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alimpa gundu.  Hamisa alitoa kauli hiyo hivi karibuni kwa hoja kwamba katika kipindi chote cha uhusiano wao hakuwahi kupata madili mengi na ya maana kama ambayo anayapata sasa baada ya kutemana naye.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Hamisa alisema tangu ameachana na Diamond ambaye alibahatika kupata naye mtoto mmoja wa kiume, amekuwa akipata madili mengi ya ndani na nje ya nchi ambayo hakuwahi kupata kipindi alipokuwa na jamaa huyo hali anayoitafsiri kama gundu.

download latest music    

“Unajua sasa hivi ninapata madili mengi hadi mimi mwenyewe nashangaa baraka zote hizi zilikuwa wapi tangu mwanzo mbona nilikuwa sipati, yaani utadhani nilikuwa na mtu ambaye alikuwa ananipa gundu, lakini sasa baada ya kumkwepa ndiyo gundu limenitoka,” alicheka na kukata simu.

Hamisa amekuwa akipitia changamoto mbalimbali kutoka kwa familia ya Diamond hadi kufikia hatua ya kupigwa na mamamkwe, kisa tu asionekane na jamaa huyo. Lakini baada ya kuachana na Diamond, mwenyewe anadai amekuwa akipata madili mengi ndani na nje ya nchi na watu wengi wanampenda na kumshauri asirudiane na jamaa huyo maana ameshadhalilishwa vya kutosha.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.