Diamond Amuiga Shahrukhan, Atoa Ufafanuzi.

Wimbo wa baila wa Diamond ft Miri-Ben Ari  unasemekana kuwa ni inspired by wimbo kwenye movie ya Jab Tak Hai Jaan(2012) picturized on Shah Rukh Khan and Katrina Kaif, ambapo baada ya wimbo huo kutoka watu walianza kusema kuwa msanii huyo amekopi kila kitu kutoka katika movie hiyo.Hata hivyo diamond hakutaka kukataa kuhusu swala hilo na hivyo amejibu kuwa ;-
.
“Sababu kubwa ya Kumpendea Sharuk Khan sio tu kuigiza bali ni Ufundi na kubobea kwake kwenye sekta ya Uigizaji wa Mapenzi katika Movie zake… Licha ya Vingi vinipavyo Furaha Lakini kuwa kwenye Mapenzi ama Kumpenda Mtu, ndio stareh yangu kubwa….Na kama ujuavyo, Unapokuwa na kajina Wengi wanakuwa wanakupenda, Wengine kwa dhati wengine kwa Matamanio…ila inapotokea anipendae nami nikampenda, basi huyo Hufaidi haswa Mapenzi yangu… na ndiomaana mara nyingi inakuwaga ni ngumu sana wengi Kunisahau pindi tutenganapo….kwani huwaga na Matendo Mengi Mazuri ya Kimahaba yanayoonekana na Yasiyoonekana gizani, kwasababu nayapenda Mapenzi, na ni Hodari sana kwenye kila taaluma ya kupetipeti… Kwa Machache nilojifunza kwenye Mahusiano nilisema, siku nikikutana na Mwanamke Mpya nitaetaka kuwa nae …kabla ya Kuianza safari, sitomwambia neno, bali nitamuekea wimbo huu wa Baila kwani Maneno yote nitayotaka kumwambia Nimeshayaweka hum….Akisha sikia na Aka-afki, Tutaianza Safari ya Mahaba”

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.