Diamond Anafanya Makosa Kumjibu Naibu Waziri:-Mngereza.

Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza amefunguka na kusema kuwa anachofanya diamond cha kujibishana na naibu waziri wa habari sio kizuri na kukifananisha kitendo hicho na kitendo cha kuitukana serikali .Diamond na naibuwaziri waliingia katika mgogoro wa kurushiana maneno baada y naibu waziri kufunga nyimbo zaidi ya  15 huku nyimbo mbili zikiwa ni nyimbo za msanii Diamond.

Mngerza anasema kuwa jambo analofanya Diamond kwa sasa ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo kama atashitakiwa na serikali pia ni kosa la kimtandao.ameongezea na kusema kuwa sio lazima mtu anapofanya kosa lazima aandikiwe barua kama yeye anavyodai.

download latest music    

Mngerza  anasema kuwa amesikitshwa sana na maneno ya diamond , kwa sababu kama angekuwa na maalalmiko angepaswa kuandika barua ili kutoa malalamiko yake na sio kwenda katika mitandao ya kijamii.

Katika kumjibu diamond, mh juliana shonza alisema kuwa hana mamlaka ya kumjibu diamond tena kwa sababu maamuzi anayoyafanya sio yake ila ni kazi ya serikali na kama ana malalamiko aandike barua, ndipo diamond alipoamua kumjibu kuwa kama yeye alianza kuyapeleka radion na kwenye mitandao na yeye hatokaa aandike barua.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.