Loading…

Diamond Aonyesha Mjengo Mpya wa Wasafi

January 11, 2018 at 15:19
Diamond Aonyesha Mjengo Mpya wa Wasafi

Haikuwa kitu raisi kwa hapo zamani mafanikio ya muziki kuonekana kama ilivyo sasa hivi, lakini pia nidhamu kubwa na juhudi ya kazi wanayoifanya kundi la Wasafi chini ya meneja wao Diamond Platinumz inatia moyo na hata kufarahisha sana na kuwa fanya wengine watamani mafanikio ya wasanii wa lebel hiyo.

Msanii  mkubwa nchini na nje ya nchi , Diamond Platinumz leo ameonyesha mjengo mpya kabisa wenye kuonyesha kuwa na thamani kubwa kabisa na kusema kuwa hayo ndio yatakuwa makao makuu ya wasanii wa lebel hiyo.

Loading...

katika ukurasa wake wa instagrama ameposti picha hiyo na kusema kuwa hayo ndio makao makuu ya wasafi ambapo ndani ya ofisi hiyo kutakuwa na sehemu ya studio ya kurekodia, ofisi za WCB, kituo cha radio cha WASAFI FM na  kituo cha Tv kitakachoitwa WASAFI TV.

Tangu Diamond ameanza musiki amekuwa mstari wa mbele sana kusaidia vijana wengine waliokuwa na nia ya kufika mbali,amekuwa akiwaongoza na kuwafanya hata wao wajulikane kimataifa,wamekuwa wasanii wenye kujituma na hata mafaniko yao yamekuwa yakionekana.

Baadhi ya picha zinazowaonyesha wasanii wa lebel ya wasafi wakiwa pamoja.

Pongezi nyingi ziende kwa Diamond na Uongozi wake lakini pia kwa wasanii wote ndani ya lebel hiyo kwa kufanya vitu vitakavyotia hamasa kwa wasanii wengine kwa sababu mafaniko yao yanaoneka katika jamii nzima.

Comments

  1. WCB ni hatari balaa

  2. Kila la kheri vijana wamefanya bidii sana

  3. Hii ni nguvu mpya jamani

  4. Mungu azidi kuwafanyia mazuri vijana wetu

  5. Kali sana simbaaaa

  6. alex hussein : April 6, 2018 at 5:32 pm

    simbaa hogera sana!

  7. tujenge hoja na vivutio vya kuwafanya wasanii wengine kazi zao wakafanyie kwenye studio ya WASAFI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.