Diamond Bado Kuoa Mpaka Miaka Mitano -Mwijaku

Msanii na mchekeshaji Mwijaku aliwahi kufunguka kuwa kamwe Diamond hawezi kuoa kwa sasa na kama angefanikiwa kuoa kama alivyotangaza kipindi cha valentine basi yeye angetoa  haja kutoka eneo alilokuwepo mpaka maeneo ya Posta.

Lakini baadae harusi hiyo ilikuwa kusogezwa mbele na  haikusemwa ni lini harusi hiyo inaweza kufanyika tena.

download latest music    

Sasa basi Mwijaku kwa mara nyingine ameongea tena na kusema kuwa msanii huyo kwa sasa hawezi kuoa kwa sababu anavyomuona anaona kabisa kuwa muda wake bado.

Mwijaku anasema kuwa kwa Diamond kuoa ni miaka mitano kutoka sasa lakini hata kuanza kuwa sereious na jambo hilo ni miaka mitatu mbele lakini sio leo wala kesho,

Mwiaku anasema “Mimi nilisema yule hawezi kuoa hivi karibuni na ni kweli, mkitaka Diamond aoe ni lazima kumpa Miaka mitano kutoka sasa, mitatu ya kufanya amaamuzi ya kuwa serious lakini kwa sasa hawezi kuoa.”

Mwijaku alisema kuwa Diamond ataoa lakini sio Tanasha kwa sababu Tanasha hana sifa za kuwa mke.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.