Diamond Kafunguka Mazito Kwenye Nyimbo Zake Mbili Mpya

Mwanamuziki machachari wa Bongo flava Diamond Platnumz ameachia nyimbo zake mbili mpya siku ya leo ambazo ni ‘sikomi’ na ‘niache’ ambapo katika nyimbo hizo Diamond amefunguka kuhusu maisha yake ya mahusiano.

Kwenye nyimbo hiyo aliyoachia mapema leo Diamond amefunguka na kuongelea yanayomsibu na mambo yanayo pelekea kumshinda mpaka kufeli katika mahusiano yake mbali mbali lakini hakuishia hapo pia aliongelea suala lake lililo make headlines kwa mwaka huu kuanzia yeye kuwa na mahusiano na Hamisa mpak kuzaa naye mtoto wa kiume aitwaye Prince Abdul au Dylan.

download latest music    

Kama ilivyo kawaida ya Diamond na nyimbo zake za mapenzi ambazo zinampelekea kulalamika. Moja kati ya mistari katika nyimbo yake ya ‘niache’ inasomeka:

Kinachoniumiza nafsi na kunisikitisha kwa watu kujishongondoa, kumbe mapenzi hisabati wakati nayazidisha mwenzangu nje unayatoa”.

Baada ya kuachia nyimbo hizo mwanamuziki kutoka label ya Wasafi Classic co. (WCB), Harmonize amefunguka na kudai kuwa WCB ndio wakali wa mziki wa Bongo fleva na wanaujua vizuri;

Muziki wa Nyumbani tunaujua na kuufahamu kiundani tunaamuaga kutia malengo kwa faida ya wasioelewa kiswahili na kukuza solo letu …WCB for life”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.