Diamond Kung’ara Kwenye Kombe la Dunia na ‘Colours’

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezidi kupaaa kwa mafanikio na kumpeleka muziki wa Bongo fleva mbele baada ya kufanikiwa kushirikishwa na Jason Derulo Kwenye wimbo wa Kombe la Dunia.

Diamond na Jason Derulo msanii kutoka Marekani wamefanya kwa pamoja wimbo unaoenda kwa jina la Colours ambao umeandaliwa na kampuni ya Coca Cola maalumu kabisa kwa ajili ya kusheherekea Michezo ya Kombe la Dunia inayotegemea kufanyika hapo baadae mwaka huu.

download latest music    

Wimbo huo ambao umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na Ma prodyuza kutoka nchi nyingine, umedhaminiwa na kampuni ya ya coca cola Tanzania.

Wimbo huo maalum wa kombe la dunia 2018 umezinduliwa leo Katika Hotel ya Hyatt, jijini Dar es Salaam, ambapo Diamond, Nahreel na msemaji wa Coca Cola wamesema wamesha uachia hewani wimbo huo hivyo unapatikana kwenye mitandao mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliweka Ujumbe kuhusu Wimbo huo:

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.