Diamond na Dillish Mathews katika skendo nzito

Mwanamuziki Diamond Platnumz amejikuta katika skendo nyingine ya kimapenzi safari hii akiwa na mwanadada mrembo kutoka Namibia Dilish Mathews ambaye ni mshindi wa Big brother Africa mwaka 2013. Inasemekana kuwa Diamond na Dillish wameonekana kwenye visiwa vya Zanzibar wakila bata kwa pamoja katika hoteli ya kifahari ya La Gemma.

Dilish ambaye aliposti kwenye kurasa yake Instagram Siku tatu zilizopita baada ya kufika kwa mara ya kwanza kwenye visiwa hivyo ambapo aliandika:

download latest music    

“First time in East Africa…I am so in love with Zanzibar #Journey of a humble dreamer #Princess #Africa”.

Baada ya muda Dillish alionekana akiposti video na picha kwenye mitandao yake ya kijamii huku akisindikiza na nyimbo za Diamond, katika video alizotuma alionekana akimuita mtu huyo aliyekuwa nae “Bae” ambapo inasemekana mtu huyo ni Diamond baada ya wote wawili kuposti picha wakiwa sehemu moja.

Baada ya habari hizi kuenea mtandaoni imekuwa skendo kwa Diamond ambaye tayari ana mpenzi wake Zari ambaye pia ni mama wa watoto wake wawili na anasemekana kuwa atakuwa baba wa mtoto wa Hamisa Mobetto ingawa ameendelea kukataa kuwa yeye sio baba.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.