Diamond Platnumz asaini dili nono

Msanii machachari wa Bongo fleva Diamond Platnumz amelamba shavu nono la kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya vinywaji vikali ya Luc Belaire ya nchini Ufaransa, ambapo Diamond amekuwa mmoja kati ya mabalozi wa kinywaji hiko.

Kupotia ukurasa wa instagram wa kampuni ya kinywaji hicho wamethibitisha kuwa Diamond atakuwa mwanafamilia mpya kwenye kuitangaza bidhaa hiyo, pia kupitia ukurasa wake wa instagram Diamond mwenyewe amethibitisha hayo.Pia ataungana na mastaa kibao duniani ambao pia ni mabalozi wa bidhaa hiyo akiwemo rapa maarufu kutoka Marekani Rick Ross ambaye pia kupitia ukurasa wake wa instagram alimkaribisha Diamond kwa kuandika “Self Made Tastes Better” caption iliyoambatana na picha ya Diamond Platnumz.

download latest music    

Dili hilo ambalo halijawekwa wazi ni kiasi gani Diamond ataingiza baada ya kusaini na kampuni hiyo, lakini huenda ikawa ni dili la mamilioni ya fedha kwani Rick Ross ambaye ni Balozi wa Belaire anakadiriwa kulipwa kiasi cha Dola za kimarekani milioni 4.1 ambayo ni zaidi ya bilioni 8 za kitanzania.

Diamond ataungana na wasanii maarufu ambao nao ni mabalozi kama Dj Khaled, Rick Ross pia mlimbwende kutoka Kenya Huddah Monroe pia ni moja ya wanafamilia wa Belaire.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.