Loading…

Diamond Platnumz Atangaza Kutoa Album Mpya

October 11, 2017 at 19:59
Diamond Platnumz Atangaza Kutoa Album Mpya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuachia albamu mpya itakayoenda kwa jina la ‘ A boy from Tandale’.

Diamond ametangaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake jioni hii kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliweka cover ya album yake (Album cover) akaambatanisha na maneno machache yaliyosomeka:

Loading...

 

“Album Soon Come… #AboyfromTandale”

Diamond yupo nchini Marekani tangu wikiend iliyopita ambapo alihudhuria Tuzo za Afrimma na aliweka wazi pia Ana shoo nchini humo. Siku ya leo video mbalimbali zilisambaa zikimuonyesha Diamond na Rayvanny wakiwa name rapper maarufu Marekani Rick Ross wakirekodi video kwa Pamoja kwa ajili ya wimbo wao mpya.

Diamond na Rayvanny wakiwa pamoja na Rick Ross.

Mapema mwezi uliopita Diamond alitangazwa kujiunga kwenye listi ya mastaa kama Rick Ross na Dj Khaled katika kuwa mabalozi wa kutangaza kinywaji cha ‘Belaire’. Mbali na hayo Diamond ameendelea kusisitiza kuwa yupo katika harakati za kuipeleka Bongo fleva mbele zaidi

Comments

  1. Hongera sana kaka,umetia bidii sana

  2. Zidi kuwakomesha kwenye game

  3. Yan nakupendea kujituma

  4. Hakuna Zaidi yako Tanzania hii

  5. Jamaa la tandale safi sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.