“Diamond Sio Mmiliki wa Diamond Karanga, Chibu Perfume Wala Wasafi Tv/ Radio”- Mange

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, mrembo Mange Kimambi ameibuka tena na kumnyooshea kidole staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai yeye ni balozi tu sio mmiliki wa mali hizo.

Tangu siku za nyuma kuna habari zimekuwa zikienea kuwa Diamond sio mmiliki halali wa Diamond karanga na hata ilidaiwa kuwa karanga hizo zilikuwa zinaitwa Diamond karanga kabla hata ya kushikiliwa na Diamond.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika haya:

Hizi karanga zinaitwa Diamond karanga miaka na miaka, wamebadilisha rangi ya paketi na kurembesha ila jina la Diamond karanga ni la miaka yote ila zinatengenezwa na kampuni ile ile ya smart. Kilichotokea ni kwamba Joseph Kusaga alinunua ubia kwenye hicho kiwanda halafu akamleta Diamond aje amfanyie promotion na ndio maana wenye karanga zao baada ya tifu wametoa siri kuwa Diamond ni balozi wao tu”.

Lakini Mange hakuishia hapo pia amedai kuwa mali nyingine tunazozitambua kama za Diamond si zake ambazo ni perfume yake inayoitwa Chibu Perfume na pia vituo vya redio na televisheni anavyotegemea kuvizindua hivi karibuni vya Wasafi Tv na Radio ambapo Mange pia amesema;

Lakini pia Wasafi Radio na Wasafi Tv Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80 na Diamond anamiliki 20% ikimaanisha kuwa uwekezaji wote wa Wasafi Radio na Tv umefanywa na Joseph Kusaga. Lakini pia Wasafi Online ambayo wasanii wanatumia kuuza nyimbo zao 95% inamilikiwa na Kusaga. Chibu Perfume 100% inamilikiwa na Johainna Kusaga, mke wa Joseph Kusaga”.

Mpaka hivi sasa sio Diamond wala uongozi wake ulioongelea tuhuma hizo nzito zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, ingawa kwa mtazamo wangu hata kama mali zote sio zake na yeye ni balozi tu haina shida ilimradi pesa inaingia kwenye akaunti kilichotakiwa ni kusema ukweli, Je wewe nini maoni yako? Tafadhali andika hapo chini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.