Diamond Ana Mapungufu Lakini Tunayavumilia :-Lavalava

Msanii kutoka katika kundi la WCB lavalva amefunguka na kusema kuwa Diamond ni bosi wao na amaekuwa akifanya nae kazi lakini diamond ni moja ya  mabosi ambao wana changamoto kubwa kwa sababu mpaka akubali kupokea nyimbo yako na kukubali kuitoa inachukua muda mrefu sana kuikagua kwa sababu anataka wasanii wake waweze kushindana vizuri katika soko la muziki.

Lavalava ambae ametoa wimbo mpya unaitwa nitake nini anajinadaa vyema kabisa kwa ajli ya wasafi Festival wiki hii huku wakiamini kuwa wazo hilo la bosi wao ni zuri kwa sababu linawasaidia kupanua wigo wao wa muziki.

download latest music    

Lavalva anaendelea kusema kuwa kuna ugumu sana kuishi ndani ya WCB kama mwanamuziki kwa sababu kuna ushindani mkubwa sana wa ndani kwa ndani baina ya wasanii wenyewe ili kupata wasanii wazuri na kutoharibu jina la kundi.

kwaio Diamond ana mapungufu yake pia lakini ana kazi kubwa sana ya kutuelimisha na kutufundisha  kwamba tusiyachukulie poa hayo mambo kwa sababu yanamadhara yake pia, 

Akiongea kuhusu Alikiba kutaka kudhamini  tamas ha lao kupitia kinywaji anasema kuwa hajui kuhusu swala hilo kwa kuwa na yeye amekuwa akilisikia tu lakini kama kweli hilo ni jambo zuri kibiashara.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.