Diamond Amtambulisha Mtoto wake Aliyezaa na Hamisa

Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amemkubali mtoto wake aliyezaa na Hamisa Mobetto na kumuweka wazi ili watu wote wamuone.

Katika mahojiano aliyoyafanya leo Diamond alikiri kuwa mtoto yule no wake na jina lake ni Dylan. Alipoulizwa na waandishi Kama Ana uhakika yule ni mtoto wake na kama amefanana naye Diamond alijibu kuwa ataposti picha baadae ili watu wamuone na waamue wenyewe Kama amefanana naye au la. Japo kuwa mama wa mtoto, Hamisa hakuweka picha ya mtoto huyo Familia ya Diamond ndio ilikuwa ya kwanza kutuma picha hiyo mitandaoni.

download latest music    

Baada ya kumaliza mahojiano hayo, Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alituma picha ya mtoto wake huyo na kusindikiza kwa maneno yaliyosema “Young Lion”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.