Diana Apanga Safari ya Maombi Gerezani kwa Lulu

Msanii wa maigizo bongo movies Diana Kimari ambae amewahi kufanya filamu nyingi na mwanadada Lulu Michael na filamu hizo zimekuwa zikiwavutia mashabiki kutokana na wasichan hoa kuonekana kuendana tabia na hata umri hivyo kuendelea kunogesha filamu hizo.Diana Kmario  amefunguka na kuelezea nia yake ya kwenda kumtembelea rafiki yake huyo gerezani na kumpelekea wadada wa kufanya nao maombezi na kumpa neno la Mungu ambalo anaamini  litakuwa likimfariji mpendwa wake.

Diana anasema kuwa kwa muda mrefu zaidi ya mara tatu  amekuwa akitaka kwenda kumuona rafiki yake huyo gerezani  lakini anakosa muda kutokana na mambo kuwa mengi na kuingiliana lakini alishapanga kuwa atapeleka kikundi cha maombi  ambacho huwa kinatoa neno kwa wafungwa na kuwafariji  kwa ajili ya kufanya maombi na Lulu Michael na anaamini kuwa tafurahi sana na kufarijika kwa hilo.

download latest music    

Sio kwamba nipo kimya simkumbuki llulu , hapana.mwisho wa mwezi huu itaenda kumuona lulu kuna wadada ambao huwa wanaenda kutoa neno kila mwisho wa mwezi kwa wafungwa  gerezani kwaio nitaenda nao na ninajua tafurahi sana.-Alifunguka mwanadada huyo.

                                                      

            moja ya picha waliowahi kuwa pamoja Diana na Lulu.

Lulu Elizabeth Michael yuko gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili jela ikiwa ni  hukumu aliyoipokea mwaka 2017 mwishoni baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusidia na kusababisha kifo cha aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba miaka takribani minne iliyopita.

Mpaka sasa ni wasanii wachache waliofunguka kuwa wamekuwa wakimtembelea Lulu gere zani, wanaokwenda huko mara nyingi ni watu wa familia yake ,ingawa pia msanii Mwijaku alikwenda na kurudi na ujumbe mzito kutoka kwa Lulu.

Moja ya filamu pendwa ambayo Lulu Michael na diana kimari walishawahi kuicheza ni ile ya foolish age na ile ya Family Disaster ambayo wamecheza na Ray Kigosi

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.