Diva Aweka Wazi Ugonjwa Unaomfnaya Asipate Mtoto, Aomba msaada wa Matibabu

Mwanadada Diva the bawse amefunguka na kueleze maumivu yake anayoyapitia kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ameambiwa kwake itakuwa ngumu sana kupata mtoto kwa sasa kutokana na blockage kubwa iliyopo katika mirija yake ya uzazi.

Diva ambae anasimulia sababu kubwa iliyomfanya kuchunguza ili kujua kama anaweza kupata mtoto ni tamaa kubwa aliyonayo sasa hivi kuhusu kupata mtoto na ndipo alijiuliza kwa muda mrefu kwanini amekuwa akinywa dawa nyingi sana lakini hawezi kushika mimba.

download latest music    

Diva ambae anasema kuwa katika maisha yake aliwahi kupata mimba lakini haikukaa miezi minne , mimba hiyo liharibika na hiyo ndio ikawa kama mwisho ya ndoto zake kubwa za kuzaa tena katika maisha yake.

Hata hivyo diva anasema kuwa kwa madatari waliomshauri na kumpima katika hospitali aliyokuwa amekwenda, wamemwambia anaweza kupata matibabu ya tatizo lake nje ya nchi lakini ndio inacost pesa nyingi sana.

Kwa sasa diva amewaomba mashabiki na watu wake wa karibu , kumuombea na kama kuna atakaeguswa na hali yake basi anaweza kumsaidia kwa chochote ili aweze kupata pesa kwa ajili ya matibabu yake nje ya nchi.

Pia Diva amewashukuru na kwataja baadhi ya marafiki zake ambao wamekuwa karibu nae hasa katika kipindi hiki cha masikitiko na maumivu makubwa akiwemo mtangazaji mwenzie wa kipindi cha shilawadu Soudy Brown .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.