Dkt. Mwakyembe- Sioni Sababu ya Kuwasuluhisha Diamond na Alikiba

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mheshimiwa Harison Mwakyembe amefunguka kuhusu ugomvi unaoendelea kati ya wasanii wawili wakubwa Tanzania Ali kiba na Diamond Platnumz ambapo amesema kuwa hatarajii kuwapatanisha tena kama alivyohaidi mwanzoni.

Wadau mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva walimuomba waziri Mwakyembe aingilie kati beef hilo la wasanii hao wawili ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawapatani huku sababu kamili ya ugomvi huo ikiwa haijajulikana huku watu wengi wakihisi bifu hilo limetokana na ushindani wa kimuziki baina yao. Bifu lao lilionekana dhahiri pale ambapo Ali kiba alitoa wimbo wa ‘Saduce me’ na kupokelewa vizuri na mashabiki wake ndipo Diamond naye alipoamua kutoa nyimbo yake mpya ya Zilipendwa masaa machache baadae ambazo ziliingia kwenye ushindani mkali kwenye mtandao wa youtube.

download latest music    

Mh. Mwakyembe amesema;

“Kama kuna ushindani kati ya Ali Kiba na Diamond ambao ni kiweledi, kitaaluma basi mimi nafikiri tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha waendelee kushindana vizuri ili tupate miziki mizito.kwa hiyo mimi nawaomba watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga”.

Pia Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa ahadi yake aliyoitoa mwanzoni ya kutaka kuwaita Diamond na Alikiba ili kufanya wimbo kwa pamoja iko pale pale kwani anaamini wote ni vijana wenye vipaji na watafanya kazi nzuri kwa pamoja ila tu kwa sasa wakati haujafika.

Mashabiki wengi wa Diamond wamekuwa wakimtuhumu Alikiba kwa kung’aa kupitia Diamond yaani kuwa asingekuwa na bifu na Diamond Alikiba asingesikika yaani anafaidika zaidi na bifu hilo.

Je wewe unaonaje je ni kweli tuhuma hizo za Alikiba kung’aa kupitia Diamond? Na je wasanii hawa wanahitaji kuendelea kuwa na bifu au wapatane tu? Tafadhali toa maoni yako hapo chini.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.