“Mwambieni Uchebe Mwanamke Hachungwi” Dogo Janja

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kunako tasnia hiyo Dogo Janja amempa ushauri mwanaume mwenzie Uchebe ambaye ameingia kwenye ndoa hivi karibuni ambapo amemfungukia na kumuasa kutomchunga mkewe Shishi.

Ikiwa miezi michache tu imepita tangu ndoa iliyofunga mwaka ifungwe kati ya Irene Uwoya na Dogo Janja ndoa iliyoongelewa sana na ndoa iliyofungwa kwa usiri Mkubwa sana.

download latest music    

Pamoja na ndoa ilikuwa ya siri na maisha yao yamekuwa ya siri sana mbali na mitandao ya kijamii lakini juzi kwenye harusi ya Shilole na Uchebe wawili hawa wameonekana hadharani kwa mara ya kwanza.

Kwenye sherehe hiyo ya ndoa ya Uchebe na Shilole ilihudhuriwa na mastaa kibao lakini Uwoya na Dogo Janja wanaweza wakawa wana mfanano mkubwa Sana na maharusi kwani wote walipitia vikwazo mpaka kufunga ndoa lakini pia walifanya ndoa za siri siri Sana.

Kwenye sherehe hiyo Dogo Janja alipiga stori na Dizzim Online na alikuwa na ushauri mmoja tu kwa Uchebe nao ulikuwa Mwanamke hachungwi:

Kiukweli harusi yangu ilikuwa ina privacy sana ila nahisi na sisi soon tutafanya kitu kama hiki tutashiriki na ndugu na marafiki lakini kikubwa nataka niwapongeze Shilole na Uchebe na ushauri wangu endapo yanatokea mambo ya kazi asimbane ampe nafasi kamkuta na kazi zake aendelee kuheshimu kazi za mwenzake na Shilole hivyo hivyo panini ninachomwambia Uchebe mwanamke achungwi sana mwanamke hachungwi kwanza unaanzaje kumchunga mwanamke”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.