Loading...

Dogo Janja na Uwoya Warushiana Maneno Mtandaoni

January 07, 2019 at 06:33
Dogo Janja na Uwoya Warushiana Maneno Mtandaoni

Msanii wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja na aliyekuwa mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya wamerushiana maneno Kupitia Mitandao ya kijamii.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya inaonekana kuzidi kuchafuka zaidi kutokana na wanandoa hao kuweka maneno ya vijembe kwenye kurasa zao za kijamii huku zikitafsiriwa kwamba wanatupiana.

Loading...

Sakata hilo limetokea siku ya jana ambapo katika ukurasa wa Instagram wa Msanii Dogo Janja, aliandika bora uonekane kwamba huna hela kuliko kutumia hela nyingi ili kuwaonyesha kwamba uko vizuri.

Katika muendelezo wa ujumbe wake, ‘hit maker’ wa Banana amerusha jiwe gizani kwa kutoa ushauri kwa mtu huyo anayedhaniwa kuwa ni mkewe, kwamba aache kuishi maisha ya kuigiza.

Acha Kufake Fake Life. Its better to live your real life hujazaliwa kufrahisha kila mmoja, Komaaa”.

Mashambulio hayo ya gizani ya Dogo Janja yanatafsiriwa kwa haraka kuwa yanakwenda kwa muigizaji Uwoya kutokana na aina yake ya maisha anayoishi na kwamba inadaiwa ni msanii anayeishi maisha ghali sana tofauti na biashara ya sanaa ilivyo kwa sasa nchini.

Share

Comments

  1. referee waves match on!

  2. leteni popcorn aisee!

  3. hapo kwa #kazatako aisee ??

  4. Hapa uwoya alikua mchokozi lazima dogo angejibu tu

  5. Vituko uswahilini!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…