Dr.Shika Akana Kuwajua Babu Seya na Mwanae

December 15, 2017 at 11:23
Dr.Shika Akana Kuwajua Babu Seya na Mwanae

Dr.Luis Shika ambae amepata umaarufu mkubwa baada ya kuvuruga ununuzi wa nyumba za tajiri lugumyi, dr.shika  amekuwa akishika vichwa vya habari vya magazeti na vyombo mbalimbali vya habari amesema kuwa hawajui kabisa Babu Seya na mtoto wake Nguza Viking  kwa sababu kipindi watu hao wanakuja nchini yeye alikuwa nje ya nchi.

Babu Seya na Nguza Viking walikuwa wasanii waliofanya vizuri  sana nchini lakini hadithi yao ya muziki ilikuja kukwama baada ya wasanii hao ambao ni Baba na mtoto kukutwa na hatia baada ya kufunguliwa kesi iliyohusu kulawiti watoto.Hata hivyo wasanii hao wametoka baada ya kupewa msamaha na raisi mwezi huu wa December tahere 9 siku ya Uhuru baada ya raisi huyo kutoa msahama kwa wafungwa zaidi ya elfu nane.

Loading...

Hata hivyo baada ya kutoka kwa wasanii hao, watu katika mitandao walianza kusema kuwa kile kipindi cha Dr .Shik kueendelea kupata kiki kimeisha kwa sababu wasanii hao wawili wameweza kukamata sana mitandao ya kijamii kwa sasa.

Simfahamu babu Seya kipindi yeye anaingia nchini tayari nilishaondoka nchini muda mrefu , lakini nafahamu nyimbo zake  ile aliyoimba baba na mwana  wanaimba na kucheza hasa ndio naifahamu vizuri.-    Alisema Dr. Shika 

Lakini pia dr.shika anasema kuwa anampongeza sana  magufuli kwa hatua na maaamuzi aliyoyachukua  kwa kuwa watu hao sasa wanaenda kuanza maisha mapya wakiwa huru kabisa.

Nampongeza sana Mh.Raisi Magufuli kwa tukio ilo la kuwatoa wafungwa na kuwapa uhuru wao ili wakanze maisha mapya.

Wametolewa wafungwa wengi siku ya msamaha wa raisi lakini  wasanii hao walipata ku-trend katika mitandao kutokana na kuwa kifungo chao kiliwagusa watu wengi nawatu wengi walitamani sana kuachiwa kwao.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.