Dudu Baya awaonya wanaopiga picha za uchi

Imekuwa kama ni desturi kwa  hivi karibuni kwa baadhi ya kina dada tena hasa wasanii wa kike chipukizi  kupiga picha za uchi na kuzipost katika mitandao ya kijamii, tena wengine wakiwa hawana nguo kabisa hata moja  huku wakijitetea kuwa iyo ni sehemu ya kazi zao zinazowaingizia kipato.Wakati hali inakuwa tofauti kwa wakaka ambao kazi zao huwa ni za heshima na huwezi kukuta mwanaume anapiga picha za uchi na kuzirusha mitandaoni.

Msanii mkongwe wa muziki nwa Bongo Fleva alikuwepo toka kitambo ambae alikuwa ni mmoja kati ya walioinua muziki wa Tanzania  Dud baya aamua kuongelea swala hilo.

download latest music    

Alipokuwa akiongea na Bongo5 na kuojiwa maoni yake kuhusu wadada wanaopiga picha za uchi mitandaoni Dudu baya alionyeshwa kukerwa sana na tabia hiyo na kulaani vibaya, Dudu baya anasema kuwa mwanamke wa dizaini iyo si mcha Mungu na hana heshima katika jamii anayoishi kwa sbabau siku zote biashara yoyote ile nzuri huwa inanunulika yenyewe.

katika maongezi yake na bongo 5 Dudu baya anasema kuwa “dunia imekuwa kama Sodoma na Gomora saivi, na ikifikia hataua ya kuweka matangazo ya biashara mitandaoni inamaana biashara imekuwa ngumu” akimaanisha kuwa wadada wa aina iyo basi kuna biashara wanaifanya ivyo wanapopost picha basi wanaitangaza biashara iyo.

Dudu baya ametolea mfano wa waganga wa kienyeji kuwa waganga wa ukweli ni wale ambao wapo kijijini na hawajitangazi, lakini unapoona bango la mganga wa kienyeji basi huyo ni muongo ,hivyo wanaopiga picha za uchi hawana uhalisia wowote.

“kama wewe ni mkali, hata ukivaa buibui utaonekana tu, uzuri wa mwanamke hauwezi kwa kutumia carolite,uzuri wa mwanamke sio kwa kuongeza makalio, wala sio kwa kujichubua ,bali ni tabia njema, nidhamu, heshima, na kumcha Mungu ndio maana hao wanaangaika mitandaoni”

Dudubaba ameishauri serikali kuhusu nini cha kuwafanya wakina dada hao wanaowekaa  picha za uchi , anasema “serikali wajaribu kuwakamata hao wanaopiga picha za uchi ,wasiseme wanaume hatujui kutongoza”

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.