Loading...

Dudubaya Apigiliwa Msumari Mwingine Baada Ya Kuwekwa Ndani

March 04, 2019 at 06:32
Dudubaya Apigiliwa Msumari Mwingine Baada Ya Kuwekwa Ndani

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amejikuta akikumbwa na Janga jingine Baada ya kuswekwa rumande.

Siku chache zilizopita Dudubaya aliwekwa ndani katika kituo cha Oysterbay Baada ya kumtolea maneno ya kejeli Marehemu Ruge Mutahaba.

download latest music    

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kufuta usajili wa Msanii, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya kuanzia  Februari 28, kutokana na utovu wa nidhamu.

Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema kuwa baraza limechukua hatua hizo baada ya msanii huyo kukamatwa na jeshi la polisi kutokana na kauli zake kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa sasa Dudu Baya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Oyster-bay jijini Dar es salaam kwa kosa la uhalifu mtandaoni.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment