Dully Sykes Kuipeleka Kampuni ya Simu Mahakamani.

Kimekuwa kilio kwa baadhi ya wasanii bongo kulalamikia kampuni za simu kuwa wanatoa baaadhi ya taarifa za muhimu kwa watu na watu hao kutumia taarifa hizo kuwatapeli watu wengine hasa mashabiki wa wasnaii hao na watu wao wa karibu.Swala gumu linakuja kuwa hata wanapotakiwa kushughulikiwa watu hao baadhi ya kampuni za simu wanakuwa wanashindwa kufanya uthibiti huo wa taarifa za watu wengine kuvuja katika mitandao.

Msanii Dully Sykes ameilalamikia kampuni moja wapo ya simu nchini na kusema kuwa kampuni hiyo imeweza kumsaidia tapeli mmoja jijini kuweza ku-renew laini yake ya simu na kuweza kuitumia kwa watu wake wa karibu kwa kuwaomba ela , kuwatapeli na hata kuwadhalilisha baadhi ya wanawake kwa kuwaomba picha za utupu.

download latest music    

Kuna mtu amere-new line yangu ya simu  akapewa ushirikiano mkubwa sana na kampuni moja ya siu nchini, huyo mtu ame-hack akaunti yangu ya faceboook na amekuwa akiomba hela kwa baadhi ya watu,amekuwa akiwaomba wanawake picha za utupu kwa kutumia line yangu , lazima niwashtaki kampuni hii ya simu kwa sababu wamehusika kwa namna moja ama nyingine.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.