Ebitoke Amebwaga Manyanga Kwa Ben Pol

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu TV, Ebitoke amefunguka kuwa ameamua tu ayabwage manyanga kwa aliyekuwa anadaiwa mpenzi wake mwanamuziki wa bongo fleva Ben Pol.

Siku za nyuma habari zilivuma kuwa Ebitoke anatoka kimapenzi na Ben Pol hii ilikuja kutokana na Ebitoke kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda Ben Pol jambo ambalo lililompelekea Ben Pol kumpokea  Ebitoke kwa mikono miwili na kumfanya mpenzi wake. Lakini siku mbili hizi kumekuwa na drama nyingi ambazo zinakuwa zinawahusisha wawili hao ambapo Ebitoke alienda kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa Ben Pol ameamua kumpotezea yaani hapokei simu zake akimpigia wala hataki kuongea naye kitendo alichodai kilimuumiza, lakini Ben Pol alipoulizwa alidai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka asipokee simu za Ebitoke sio kuwa anampotezea bali ni kwa sababu yupo kwenye tamasha la fiesta hivyo sehemu nyingi wanazoenda hakuna mtandao na pia yupo na ubize kidogo.

download latest music    

Kwenye mahojiano na TBC 1 katika kipindi cha Papaso, Ebitoke aliweka wazi kuwa kutokana  na ubize wa Ben Pol na malengo yake  ameamua tu kumuacha;

Unajua mapenzi ni hisia, nahisi ni kama nilikuwa kama namlazimisha lakini nimegundua siwezi nikakosa furaha nikashindwa kufanya baadhi ya malengo yangu, kwa hiyo nimeamua kumuacha afanye maisha yake, ameniacha na mimi nimemuacha tunimeamua kutulia nifanye mambo yangu”.

Amefunguka Ebitoke, lakini pia amesisitiza kuwa kuanzia hivi sasa hatarudia kosa la kumtangaza mpenzi wake kwenye mtandao wa kijamii tena yaani hata akipata mpenzi mpya hawezi kuja kumtangaza hadharani ni kitu alichojifunza ni kukaa kimya kuhusu uhusiano wake.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.