Ebitoke Aongelea Kuhusu Ukimya Wake

November 14, 2017 at 11:06
Ebitoke Aongelea Kuhusu Ukimya Wake

Alipoanza kujulikana katika tasnia ya sana alikuwa ni moja ya wasanii wasioisha kutajwa midomoni mwa watu lakini hivi karibuni ameonekana kupoa kidogo , badhi ya mashabiki wameanza kusema kuwa labda na yeye amefulia na zile kiki  alizokuwa anatafuta zimekwisha lakini msanii huyo wa maigizo ya vichekesho kwa jina la Anastazia Xavery akijulikana kwa jina  maarufu la Ebitoke amekana swala hilo na kusema kuwa yupo sana katika game na wala hategemei kuacha kazi yake kwa sabau ni kipaji alichozaliwa nacho.

Ebitoke amesema kuwa tangu amezaliwa, amezaliwa kwa ajili ya kazi ya kuchekesha kwaiyo ni kitu kilichopo katika damu yake na hawezi kuacha na kwa sasa ana madude mengi ya hatari bado hajayaonesha  ila anaomba watu wamvumilie kwa sababu amekuwa akitingwa na majukumu ya hapa na pale lakini ataibuka hivi karibuni.

Loading...

ha! ha! haa!  mimi sio rahisi kupotea kihivyo kama watu  mnavyofikiria aisee, niko na madude mengi sana ya hatari  bado sijayaachia, sema kuna baaadhi ya majukumu ya kikazi kwa sasa ninayafanya.-Alifunguka Ebitoke

juzi juzi katika moja ya majukwaa ya matamasha ya fiesta ambalo hivi karibuni linafikia ukingoni Ebitoke alionekana katika jukwaa akiwa na msanii Ben Pol wakiombana na msamaha na kutangaza kusameheana na kurudiana hivyo zile tetesi za kuwa wameachana kufutika tena masikioni pa watu ambapo kwa muda kidogo wawili hao walionekana kuwa mbalimbali na kusemekana kuwa walikuwa wamegombana.

Ingawa Ben Pol mwenyewe amekuwa akikanusha habari za kuwa na mahusianao na mwanadada huyo lakini Ebitoke kila siku amekuwa akisema anampenda sana Ben Pol.

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
CeciliaVictorBarbraNancyMercy Recent comment authors
newest oldest most voted
Mercy
Guest
Mercy

Ebitoke balaa

Nancy
Guest
Nancy

Basi amsha madude

Barbra
Guest
Barbra

Shughuli za jamii ni nzuri sana

Victor
Guest
Victor

Nakaoendaga sana haka kadada..kazuri sana kwenye kuigiza

Cecilia
Guest
Cecilia

Poa basi,hivi Ben Pol mlitemana kwa nini?


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.