Ebitoke: Bado Nampenda Ben Pol

Mchekeshaji kutoka Timamu tv Ebitoke amefunguka na kudai kuwa pamoja na kwamba alishasema ameachana na mwanamuziki Ben Pol lakini bado anampenda.

Ebitoke aliweka wazi hisia zake na kukiri kuwa anavutiwa na Ben Pol na kumtongoza mpaka baadae kuanza naye mahusiano ya kimapenzi ingawa kulikuwa kuna utata fulani wenyewe walidai kuwa ni wapenzi. Mwezi uliopita Ebitoke alidai kuwa Ben Pol amemuacha na kila akijaribu  kumpigia simu anakuwa hapokei akimtafuta anampuuza na kudai kuwa ameamua kuachana naye na kutafuta mwanaune mwingine.

download latest music    

Wikiendi iliyopita kulikuwa kuna tamasha la Fiesta ambalo liliwakutanisha wasanii wote wakubwa wa Tanzania moja wa wasanii waliofanya shoo kubwa ni Ben Pol ambaye alipata shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki ambapo alimuita muigizaji Tausi akaigiza naye kama make wake lakini Ebitoke akatokea na kudos Ben Pol ni wake hapo ndo mahaba mazito yalionekana live.

Baada ya tukio hilo Ebitoke alifanya mahojiano na Millard Ayo Tv Ebitoke amesema kuwa bado anampenda Ben Pol na kwa sasa wako vizuri na wamesamehana kwamambo yote yaliyotokea huko nyuma.

Hivi sasa mimi na Ben Pol tuko vizuri tunaongea kwenye simu kama kawaida hapo katikati tulipitia matatizo matatizo fulani lakini sahivi tuko vizuri ingawa sahivi nimejifinza mambo mengi kuhusiana na mapenzi yaani sasa hivi sitampa moyo wangu kwa asilimia Mia moja yaani mguu moja ndani mwingine nje ili akinitenda nisiumie sana”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.