Loading…


<--! Medium Rectangle -->

Ebitoke: Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani

August 11, 2017 at 13:06
Ebitoke: Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani

Siku chache zilizopita, Ben Pol alisema kuwa hataki aulizwe kuhusu mahusiano yake na mchekeshaji Ebitoke. Msanii huyo alieleza kuwa anajiusisha na mambo ya muziki kwa sasa na hangependa kuongelea mambo yake binafsi.

Ebitoke amedhibitisha kuwa yeye na Ben Pol bado ni wapenzi ila hawataki tu kuweka mapenzi yao hadharani. Akiongea na Times FM, Ebitoke alisema mipango walionayo kwa sasa ndio inapelekea kutoonekana pamoja kwa sasa na kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.

Loading...

Ben Pol na Ebitoke

“Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo. Tunamipango mingi, kwanza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote na ameniaidi lazima ahakikishe natimiza malengo yangu na ameona mimi bado ni mdogo ananifundisha kila kitu jinsi gani nikue kwenye hii tasnia na the way hii mitandao ya kijamii ilivyo na maneno ya watu yalivyo,” alisema Ebitoke.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere