Ebitoke- Namchukia Sana Mange Kimambi

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke amefunguka na kuweka wazi kuwa hampendi kabisa Mwanaharakati wa mambo ya siasa mitandaoni Mange Kimambi.

Kama utakumbuka siku za nyuma Ebitoke alishawahi kuingia Kwenye headlines baada ya Mange kutangaza kuwa Anatembea na bosi wa Timamu Tv ambaye ni mume wa msanii mwenzake Mama Ashura na hadi kusababisha Mama Ashura kufukuzwa.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Ebitoke aliulizwa anamchukuliaje Mange Kimambi na mara moja alitiririka jinsi anavyomchukia:

Yaani katika watu ambao siwezi kiwazungumzia ni huyo, Kwanza huyo Dada mimi simpendi, ameshawahi kuongia kwenye anga zangu lakini hata kabla ya hapo nilikuwaga simpendi.

Halafu siwezi kumkubali yule dada maana hanisidii kitu chochote mimi naona anawasaidia watu wengine, Mimi sipendi mambo yake na wala sikapendi na wala sipendi vimtu vinavyoongea sana “.

Lakini pia Ebitoke amesisitiza taarifa alizozieneza Mange hazikuwa na ukweli hata kidogo kwani yeye na Mama Ashura wako vizuri kabisa ingawa sio marafiki.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.