Loading...

Esma Platnumz Athibitisha Mahusiano Ya Petit Man na Karen

October 26, 2018 at 08:14
Esma Platnumz Athibitisha Mahusiano Ya Petit Man na Karen

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameanika mahusiano ya mumewe wa zamani Petit Man na msanii wa Bongo fleva Karen Gadner.

Miezi michache iliyopita Esma na aliyekuwa mume wake na mzazi mwenzake Petit Man walitangaza kuachana baada ya miaka michache ya ndoa lakini muda mfupi baadae tetesi za Petit kuwa Kwenye Mahusiano na Karen zilianza kusambaa.

Loading...

Lakini Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma amefanya kama kuweka wazi Mahusiano hayo ambapo aliulizwa endapo Mtoto wake na Petit anamkumbuka baba yake ambaye kwa sasa hawaishi pamoja ndipo alipojibu:

Anamkumbuka tena sana tu sasa atafanyaje na baba yake ndio kashanogewa na penzi jipya la mtoto wake Gadner jamani mbona mnajifanya hamjui wakati mnajua kila kitu kwani hamjui mbona hata wanaishi pamoja jamani sio siri tena”.

Lakini pia Esma ameweka wazi kuwa hana mpango wa Kuolewa Tena kwa sasa lakini ametaja vigezi anavyovitaka kwa mwanaume ili Awe naye Kwenye Mahusiano:

Napenda mtu mzima ambaye kashamaliza ujana halafu ‘Gentleman’ nitulie naye utoto utoto hapana kwa sasa maana kinyago ukichonge mwen-yewe mwisho wa siku kinakutisha mwenyewe sitaki mimi nimejifunza”.

Share

Comments

  1. Afadhali hivyo hujaongea na machungu

  2. Nice. Be the bigger person.

  3. Yaani kakuacha kaenda mtoto mchanga. Pole

  4. Yataka moyo mami. Pole

  5. Hio ni karma ya kupenda kuingilia mahusiano ya ndugu yako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…