Esma:Sipendi Kumtegemea Diamond

Dada wa msanii  mkubwa nchi , Esma Platinumz ameesema kuwahataki kuwa tegemezi kwa kaka yake hata siku moja pamoja na kwamba wawili hao ni ndugu na kaka yake ana uwezo mkubwa wa kumsaidia kifedha na hata kumtangaza kwa watu mbali mbali lakini yeye anataka asimame peke yake ili aweze kuwa na uchungu wa mafanikio.

Esma ambae hapo mwanzoni alikuwa karibu sana na kaka yake na hata kuwa natembea nae baadhi ya nchi alikuja kupunguza mahusiano hayo na kuanza kufanya biashara zake mwenyewe ili kusimama mwenyewe kimaisha, ingawa kuna wengi walikuwa wakisema kuwa mahusiano hayo yalipungua kwa sababu halikuwa hataki uhusiano wa kimapenzi na kaka yake lakini hii haikumfanya  hawasikilize sana watu katika mitandao.

download latest music    

Wapo waliofikia hatua ya kusema kuwa Esma ni lazima atumie umaarufu wa kaka yake kufanikiwa na kuunganishwa na waut mbalimbali lakini mwanadada huyo alikataa na kuanza kufanya biashara zake mwenyewe.

Akiongea na gazeti la Amani, Esma anasema kuwa siku zote anataka kuwa anajivunia mafanikio yake mwenyewe na hataki kumsumbua kaka yake au wifi yake Zari kwa sababu ya umaarufu wao.

najua kabisa kuwa kaka yangu na wifi yangu zari ni watu maarufu sana katika mitandao,lakini nilitamani sana katika mafanikio yangu niwe nimesimama mwenyewe  ili nijue changamoto zake katika kufanikiwa kwangu na kweli nimeweza.

Esma ambae kwa sasa anauza vitu mbalimbali kama vipodozi na mavazi amekuwa ni moja ya wafanyabiashara wanaofanikiwa sana katika biashara yake.Esma na Diamond ni ndugu wa kuchangia mama .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.