Fahamu: Dawa Za Nywele Ni Hatari Kwa Afya Ya Kizazi Kwa Wanawake

Ni wanawake wengi wanaomini kuwa  dawa za nywele ndio  inayosaidia sana katika urembo wa nywele zao , hii yote ni kwa sababu unapoweka dawa kwenye nywele ulainika sana na kuonekana zenye mvuto.Lakini je ni mara ngapi wanawake wamekuwa wakifatilia dawa wanazoweka na madhara yake ambayo yanweza yasipatikane mara moja.Madaktari wanathibitisha kuwa utumizi ya dawa za nywele kwa wanawake zinasababisha kuleta uvimbe katika uzazi hasa kupitia majeraha ambayo mwanamama anayapata wakati wa kupaka dawa.

Moja ya madaktari kutoka Tanzania katika hospitali ya Ilala Dk.Lauren  Chipata , alishawahi kufanya utafiti na kugundua kuwa dawa za nywele na vipodozi vyenye kemikali vinazalisha kemikali inayochochea kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa oestrogen mwilini, ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kukua kwa fibroids au myoma.

download latest music    

Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi, na wakati mwingine hata kwa harufu tu unayovuta ya kemikali hizi,na kusababisha uzalishaji wa vichocheo vya oestrogen kwa wingi na kuleta fibroids”-anasema Dk. Chipata

Daktari huyo anasema kuwa kukua kwa fibroids hutokea sana kipindi mama anapokuwa katika kipindi cha uzazi, yaani kabla hedhi haijakoma na ndicho kipindi ambacho wakidada wengi wanakuwa wamejikita katika maswala ya urembo pia.

kwa uhakika wa utafiti huu, Dk.Chipata alitumia wanawake wa kada tofauti wenye nywele zenye dawa na wale wasiotumia ili kupata majibu yatakayo leta athari kwa jamii.Hata hivyo mamalaka ya chakula na dawa kwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele sana katika kukamata na kukatza matumizi na uingizaji wa dawa na vipodozi vyenye kemikali ili kupunguza matatizo kama hayo katika jamii zetu.

Utafiti mwingine uliofanyika huko Marekani mwaka 2012 na Dk.Lauren Wise  na wenzake na kisha kuchapishwa katika jarida moja la afya nchin karekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vyenye kemikali ikiwepo na dawa za nywele zimekuwa na kemikali nyingi zinazosababisha kuzalishwa jwa vichocheo vya oestrogen ambavyo husababisha uvimbe kwenye kizazi na pia katika mji wa mimba.

Dk.Wise aliwafatilia wanawake takribani 23580 ambao wamekuwa wakitumia dawa hizo na kuangalia wameungua mara ngapi, wameanza kuzitumia kwa muda gani na wakati wa kupaka wamekaa nazo kwa muda gani ambapo wanawake 7146 walikutwa  na uvimbe kwenye uzazi baada ya kupimwa na ilibidi kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo Dk.Wise anasema kuwa bidhaa za dawa za nywele zilizoandikwa no lye relaxer  zinadaiwa kusababishwa madhara zaidi kuliko zile zilizoandikwa lye relaxer

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.